Cancion : Amua Artista : Hesian Album : Hesian Url : https://www.letras10.co/letra-amua-de-hesian [Intro] Nduati: Haya! Habari ya leo? Response: Njema Nduati: Basi jina langu ni Nduati na mimi leo nitakuwa mwalimu wenu Basi somo la leo hili, si somo sana la Kiswahili, si somo sanasana la dini, ila ni somi la kimaisha Mko tayari lakini? Response: Naaaaam [Verse 1] Achana na wahenga (waambie) Ati haba na haba hujaza kibaba Unafaa kusikia ya Yesu Haba na haba ilijaza wababa elfu tano Achana na wahenga Kidole kimoja hakivunji chawa (sawa) Unafaa kusikia ya Yesu Neno moja; kila kitu inafanywa sawa Hapo mmelearn nini? Yesu ananijali mimi Yeye ako na nguvu zaidi Na hizo nguvu zitanifaidi Yesu ndio kusema nani anaweza finya mute? Na akishasema nani anaweza refute? So acha Yesu awe ile tune unaskiza Zile maneno huleta nuru kwa giza [Hook] Utaskiza nani? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo Sema utamskiza nani wewe? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo Utaskiza nani? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo Ah! Wee... Utaskiza nani? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo [Verse 2] Achana na wahenga (waambie) Ati aliye juu mgonje chini Unafaa kusikia ya Yesu Akishakuinua hakuna aweza kuweka chini Achana na wahenga Mtaka cha mvunguni sharti ainame Unafaa kusikia ya Yesu Mtaka cha mbinguni ni rahisi sharti aamini Hapo mmelearn nini? Yesu ananidhamini Kazi tu ni kuamini na mbinguni ni nyumbani salama salmini Yesu ndio kusema nani anaweza finya mute? Na akishasema nani anaweza refute? So acha Yesu awe ile tune unaskiza Zile maneno huleta nuru kwa giza [Hook] Utaskiza nani? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo Sema utamskiza nani wewe? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo Utaskiza nani? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo Ah! Wee... Utaskiza nani? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo [Verse 3] So, wahenga ni wengi But Yesu ndiye mhenga mkuu (waambie) Ye ndio usipomskiza Buda! Utavunjika guu Kwa hivyo skiza tu za Yesu Zingine za dunia hazifai (For example) Hakuna vile nitaskiza nyongwa na Mungu ashasema ananipa uhai Irony ni that wanaitwa the Kansoul But hizo ndizo counsel tunafaa kucancel Alafu tunakimbilia neno la Bwana mbio sana ni kama nyuma kuna (kanjo) city council Nani anaweza finya mute? Nani anaweza refute? So acha Yesu awe ile tune unaskiza Zile maneno huleta nuru kwa giza [Hook] Utaskiza nani? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo Sema utamskiza nani wewe? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo Utaskiza nani? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo Ah! Wee... Utaskiza nani? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo Utaskiza nani? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo Sema utamskiza nani wewe? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo Utaskiza nani? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo Ah! Wee... Utaskiza nani? Amua leo! Ha! Ha! Amua leo ========================== Letra descargada de Letras10.co ==========================