Cancion : Nalivua Pendo Remix Artista : Nandy Album : Nalivua Pendo Remix Url : https://www.letras10.co/letra-nalivua-pendo-remix-de-nandy Oh oh oh oh Leo nalivua pendo nililopenda zamani Nabadilli wangu mwendo nami niwe furahani Nimechoshwa na skendo, vita na purukushani Kweli asiyejua pendo apendwapo hapaoni Nilimpa kwa kishindo penzi lote la moyoni Raha na wingi uhondo sikumnyima mwandani Ameyavunja kwa nyundo mwenzenu sikuamini Leo nalivua pendo nirudi yangu thamani Nainua mikono baba kitambaa cheupe Ishara ya mapenzi baba ooh zimora Wewe na mi zimora baba ua langu la moyo Haya yote ni tisa tuu moja jaza pekee Ada ya mja hunena, ungwana ni kitendo uuh Hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo Wewe na mi zimora baba ua langu la moyo Haya yote ni tisa tuu moja jaza pekee Nimehitimu msondo msondo wa kizamani Nikahusiwa upendo upendo siri yake nini Nimefundwa kimitindo na starehe za chumbani Kupendana ni matendo mtendeane hisiani Kweli mchezea jando mapenzi kwake ni nini? Bora niyapige tindo (turururu) Mimi nawe buriani Nainua mikono baba kitambaa cheupe Ishara ya mapenzi baba ooh zimora Wewe na mi zimora baba ua langu la moyo Haya yote ni tisa tuu moja jaza pekee Ada ya mja hunena, ungwana ni kitendo uuh Hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo Wewe na mi zimora baba ua langu la moyo Haya yote ni tisa tuu moja jaza pekee Wewe na mi zimora baba ua langu la moyo Haya yote ni tisa tuu moja jaza pekee Chika chika chika chika chika Mwasiti Chika chika chika chika chika chika Haya yote ni tisa tuu Zimora zimooora Zimoraa oooh baba ========================== Letra descargada de Letras10.co ==========================